RAIS KIKWETE AZINDUA OFISI YA TRA KARATU

0 comments

http://2.bp.blogspot.com/-U7YyUfSOQGI/U1aNnSiKfQI/AAAAAAAFcVE/bMARJjJq0q0/s1600/D92A6757.jpgRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunu kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kufungua rasmi ofisi ya Mamlaka ya mapato Wilaya ya Karatu leo mjini Karatu.picha na Freddy Marohttp://2.bp.blogspot.com/-DbmI-nR_Yt4/U1aNc_c3LQI/AAAAAAAFcU8/1BAz4Ib9wxg/s1600/D92A6774.jpgRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mbumge wa Karatu mchungaji Israeli Nase(Watatu kushoto),Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe(Wapili kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo(kushoto) na Mkurugenzi wa Utumishi na utawala wa TRA aliyemwakilisha Kamishna mkuua wa TRA Bwana Abubakari Kunenge(wapili kulia) na kulia ni mwakilishi wa ofisi ya TRA Mkoa Bi.Caroline Ntinku.
Categories:

BAADA YA DAVID MOYES KUTIMULIWA MAN UNITED LEO, HUYU NDIYE KOCHA MPYA WA TIMU HIYO

0 comments
Kutokana na kutofanya vizuri chini ya uongozi wake David Moyes hatimaye leo April 22 Manchester United wamemtangaza Mchezaji wa siku nyingi wa Manchester United Ryan Giggs kukabidhiwa  kwa muda mikoba ya David Moyes aliyetimuliwa kazi leo

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA SIMIYU KUFUATIA AJALI YA BASI LA LUHUYE

0 comments
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Paschal Mabiti,kuomboleza vifo vya watu 11 ambao wamepoteza maisha yao katika ajali ya basi iliyotokea mkoani humo Jumatatu, Aprili 21, 2014.

Katika salamu hizo, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha  kuwa ajali zabarabarani zinaendelea kuchukua maisha ya watu wasiokuwa na hatia.

“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya ajali hiyo ambayo nimejulishwa kuwa imetokea katika Kijiji cha Itwimila katika Wilaya ya Busega katika Mkoa wako wa Simiyu wakati basi lililokuwa linasafiri kutoka Tarime, Mkoa wa Mara kwenda Mwanza kupitia Simiyu lilipoacha njia na kugonga nyumba kabla ya kupinduka.”

Amesema Rais Kikwete: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi na najiunga nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu. Aidha, kupitia kwako, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia zote ambazo zimepoteza wapendwa wao katika ajali hiyo. Naungana nao katika kuomboleza wapendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aziweke peponi roho za marehemu.”

Rais Kikwete vile vile ametoa pole kwa wote ambao wameumia katika ajali hiyo, akiwaombea wapone haraka na kurejea kwenye shughuli zao za kujiletea maendeleo.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Aprili,2014
 

MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 22, 2014

0 comments

000_09d56.jpg
00_edadc.jpg
0_772df.jpg
1_f87b6.jpg
2_bc7a6.jpg
4_28373.jpg
5_ce9a6.jpg
006_689a8.jpg
06_f582a.jpg
9_661f9.jpg
10_b25b2.jpg
11_a148e.jpg

NDUGU WA WALIOZAMA NA MELI HUKO KOREA KUSINI WAPAMBANA NA POLISI

0 comments
Jamaa wa baadhi ya waathiriwa 250 wa ajali ya Ferry nchini Korea Kusini ambao bado hawajapatikana, wamekabiliana na polisi.

Jamaa hao wanalalamikia kile wanachosema ni kujikokota kwa waokozi wanaowatafuta waathiriwa hao.
Usiku kucha, wapiga mbizi walipata miili 17 zaidi baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya Ferry hiyo iliyozama kwa mara ya kwanza.

Walinzi wa bahari katika pwani ya nchi hiyo, walishindwa kueleza ni sehemu gani hasa ambapo miili hiyo ilipatikana ndani ya ferry hiyo baada ya kushindwa kuona vyema wakiwa chini ya bahari.

Meli hiyo ilizama siku ya Jumatatu ikiwa imewabeba watu zaidi ya mia nne wengi wakiwa wanafunzi wa shule.

Mawimbi makali na hali mbaya ya hewa inaathiiri shughuli ya kuwatafuta waathiriwa.

Waendesha mashitaka wanasema kuwa wakati wa ajali hiyo kulikuwa na nahodha mwingine asiye na uzoefu aliyekuwa ameshikilia usukani wa meli hiyo.

Nahodha huyo alikamatwa pamoja na nahodha wa ferry hiyo na wafanyikazi wengine.

chanzo:bbc swahili

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 21, 2014

0 comments
9_b71b7.jpg
2_50d43.jpg15_2c371.jpg
3_f3c93.jpg14_9baf4.jpg
4_e9150.jpg11_3475b.jpg
5_b678f.jpg
6_9ad76.jpg
7_e8257.jpg
8_41f06.jpg
10_1df7a.jpg
12_dbeb4.jpg
13_8ee1e.jpg
IMG-20140421-WA0003_7a44e.jpg
IMG-20140421-WA0006_51a61.jpg
IMG-20140421-WA0008_b5c29.jpg
IMG-20140421-WA0010_7521d.jpg
IMG-20140421-WA0012_303ef.jpg
IMG-20140421-WA0013_71133.jpg
IMG-20140421-WA0014_c1e6f.jpg

Categories:


TAMASHA LA PASAKA LATIKISA UWANJA WA TAIFA, MEMBE ASEMA WANANCHI WATAAMUA SERIKALI IPI WANAITAKA

0 comments
 Mchungaji mtarajiwa Masanja Mkandamizaji akifanya vitu vyake jukwaani
 Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Tamasha la Pasaka lililofanyika jana kwenye uwanja wa Taifa akizungumza na mashabiki mbalimbali waliojitokeza katika tamasha hilo na kuwaomba kuwa watulivu wakati huu wa mchakato wa katiba mpya akisema uamuzi mtautoa ninyi, ni serikali gani mnaiihitaji iwe moja, Tatu au Mbili nyinyi ndiyo mtaamua na sisi tutakipitisha kile mlichokiamua, Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama na katikati ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mh. Angela Kairuki.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
 Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo akicheza na mashabiki wake wakati alipokuwa akifanya vitu vyake  kwenye uwanja wa Taifa jana.
 Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti akiimba jukwaani jana.
 Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo akicheza na kwa mbwembwe wakati alipokuwa akifanya vitu vyake  kwenye uwanja wa Taifa jana.
  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete akiongozwa kuelekea jukwaani na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama BONYEZA HAPA KWA PICHA ZAIDI


SALAMU ZA MWISHO WA MSIMU TOKA KWA WEKUNDU WA MSIMBAZI

0 comments
 http://4.bp.blogspot.com/-IQg1X6KZyGA/U1T9oQc2KGI/AAAAAAABmcQ/9EhzMVb7mp4/s1600/index.jpg 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UONGOZI wa Simba SC unapenda kuwashukuru wanachama na washabiki wake wote hapa nchini kutokana na mshikamano mkubwa waliounyesha wakati wa kuelekea kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu.

Ingawa matokeo hayakuwa mazuri siku zote, lakini mapenzi ambayo washabiki walionyesha kwa klabu yao lilikuwa ni jambo la faraja kwa uongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji.


Wachezaji wa Simba pia wameelezea kufurahishwa kwao na namna washabiki waliokwenda kwenye Uwanja wa Taifa kutazama pambano la Watani wa Jadi Jumamosi iliyopita, walivyowashangilia kwa dakika zote tisini.

Uongozi wa Simba unapenda kuwaahidi washabiki wake kwamba utafanya kila uwezalo kuhakikisha kwamba klabu inajiandaa vya kutosha kufanya vizuri msimu ujao.


Makosa ambayo yalisababisha timu isifanye vizuri msimu uliomazika yatatazamwa na kufanyiwa upembuzi yakinifu ili yasijirudie tena katika msimu unaokuja na mingine.


Simba SC inaamini kwamba wanachama wake watakuwa bega kwa bega na uongozi kuhakikisha kwamba mambo anakwenda vizuri msimu ujao.

MAPATO

Msimu huu ulikuwa na changamoto kubwa sana za kimapato. Katika mechi baina ya Simba SC na Ashanti iliyochezwa jijini Dar es Salaam, mgawo kwa Simba SC ulikua ni zaidi kidogo ya shilingi laki tatu. Hii ni rekodi katika historia ya Simba.

Hili lilisababishwa zaidi na kutofanya vizuri kwa timu. Hata hivyo, uongozi ulijitahidi kwa kadri ilivyowezekana kupambana na changamoto hizi kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani na ubunifu.

Pamoja na changamoto zote hizo, uongozi ulijitahidi kuisimamia timu na hata katika mechi ya Watani wa Jadi iliyofanyika Jumamosi iliyopita, timu iligharamiwa na viongozi waliopo pasipo kupata msaada wowote kutoka nje ya uongozi.

Kupitia uzoefu uliopatikana msimu huu kwenye eneo la mapato, uongozi sasa utabuni namna nyingine za kuongeza mapato ili kupambana na changamoto za kupungua kwa mapato ya milangoni.


TIMU

Mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu, klabu imevunja kambi na wachezaji wote wamepewa ruhusa ya kupumzika hadi katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu ambapo timu itaanza mazoezi kujiandaa na msimu ujao.


Na kama ilivyo katika vitabu vya Sayansi ya Michezo, Simba itafanya mazoezi ( Pre Season) kwa walau wiki sita kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu msimu ujao. Simba haitakuwa na mechi yoyote ya kirafiki na wala haitashiriki mashindano yoyote yatakayokuwa yameandaliwa katika kipindi cha kati ya mwezi Juni au Julai; labda kama benchi la ufundi litaona inafaa.


KOCHA LOGARUSIC

Uongozi wa Simba unaendelea na mazungumzo na kocha wake, Zdravko Logarusic, kuhusu kumuongezea mkataba wake na mazungumzo hayo yatafikia tamati mwishoni mwa wiki hii.

Klabu itatoa tamko rasmi kuhusu endapo itaendelea au haitaendelea na mkataba wake na kocha huyo baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo. Kwa sasa, haitazungumzia lolote kuhusu hilo hadi mwishoni mwa wiki hii.


Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Katibu Mkuu
Simba SC

NDUGU WANAOKULA NYAMA ZA MAITI WAKAMATWA

0 comments
Watu wawili wanaotuhumiwa kula nyama za binadamu wamekamatwa baada ya kichwa cha mtoto wa miaka mitatu, kukutwa katika nyumba wanayoishi nchini Pakistan.


Polisi waligundua tukio hilo la kutisha na kuwakamata watuhumiwa Mohammad Arif Ali (35) na mdogo wake Mohammad Farman Ali mwenye miaka 30.

Kwa mujibu wa gazeti la mtandaoni la Dailymail, wanandugu hao wanaotoka katika mji mdogo wa Darya Khan wamewahi kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kula nyama za binadamu. Waliachiwa huru baada ya kumaliza kutumikia adhabu hiyo mwaka jana.

Arif na Farman walikamatwa na kuswekwa rumande wakati uchunguzi ukiendelea, baada ya tukio hilo lililowavuta wengi na kutikisa tena eneo hilo.

Miaka mitatu iliyopita ndugu hao walifukua zaidi ya miili 100 ya maiti katika makaburi yaliyopo karibu na kijiji chao kisha kuzitumia maiti hizo kama asusa.

Mkuu wa Polisi katika eneo hilo, Ameer Abdullah alisema maofisa wake wa polisi waliamua kuvamia na kufanya upekuzi katika eneo hilo, baada ya majirani kulalamika kwamba kuna harufu mbaya ambayo imekuwa ikitoka katika nyumba waliyokuwa wakiishi.

“Wakazi hao waliifahamisha polisi baada ya kusikia harufu mbaya ikitokea katika nyumba waliyokuwa wakiishi watu hawa,” alisema Abdullah.

Abdullah alisema: “Tulifika katika nyumba hiyo siku ya Jumatatu asubuhi na kufanya upekuzi kabla ya kukiona kichwa cha mtoto wa miaka mitatu.

“Baada ya kugundua kitu hicho kinachotisha, tulimkamata mmoja wa ndugu hawa Mohammad Arif na alitupatia ushirikiano hadi tulipomweka kizuizini ndugu yake,” alisema Abdullah.

Alisema jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi ili kung’amua iwapo kuna makaburi mengine yamechimbwa na watu hao kijijini hapo au katika vijiji vya jirani.

Baada ya kuulizwa maswali mengi na polisi, ndugu hao walikiri kula nyama za watu na kueleza ukweli namna walivyokuwa wakitengeneza mlo huo. Kwa kuwa Pakistan haina sheria zinazohusu ukatili wa maiti, huenda haitakuwa rahisi kwa wawili hao kufungwa jela

TAARIFA KAMILI YA AJALI YA BASI LA LUHUYE LILILOUA WATU 12 HUKO SIMIYU

0 comments
Watu 11 wamepoteza maisha  papo hapo na mwingine mmoja kufariki  dunia akiwa njiani akipelekwa hospitali  ya rufaa ya Bugando,baada ya kutokea ajali mbaya ya gari iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Luhuye T 410 AWQ lililokuwa likitokea Tarime Mkoani Mara kwenda jijini Mwanza.  
Basi hilo liligonga nyumba kisha kupinduka leo saa tano na dakika 10 asubuhi  katika barabara ya Mwanza – Mara katika kijiji cha Yitwimila kata ya Kiloleli wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.   
Mbali na watu 12 kufariki dunia pia watu 60 wamejeruhiwa ambapo imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo kuwa  ni mwendo kasi wa sasi hilo ambapo dereva wa alishindwa kumudu gari hilo likiwa katika kasi na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa pembezoni mwa barabara na 
kupinduka.   
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, mkuu wa Mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti amesema miongoni mwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo wanawake ni 5 na wanaume 7.   
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema kabla ya kutokea kwa ajali  hiyo basi hilo lilianza kuyumba na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa kando kando ya barabara hiyo. 
  Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Dk Athuman Pembe alithibitisha kupokea majeruhi 60 pamoja na maiti 11.   
Amesema kati ya majeruhi hao 25  hali zao siyo nzuri wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, na kwamba hali za majeruhi waliobaki katika hospitali hiyo zinaendelea vizuri na tayari wengine wameanza kuruhusiwa.   
Jeshi la polisi mkoani Simiyu limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

MIMI NA RIDHIWANI KIKWETE HATUJAMTUKANA MHE. LOWASSA - MEYA JERRY SILAA

0 comments
Majibu ya Mh.Jerry Silaa kuhusiana na hili swala. Source ya majibu ni facebook page ya Jerry Silaa.

Nimepokea kwa Masikitiko makubwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni ikidaiwa ni mawasiliano baina yangu na Ridhiwani Kikwete, Mjumbe wa NEC na Mbunge mteule wa Jimbo la Chalinze.

Ingawa si tabia yangu kukanusha mambo yaliyotengenezwa kwa sababu anazojua muandaaji lakini kwa idadi ya simu nilizopokea kwa faida ya wengi ni bora niseme yafuatayo.

1.Kwa wanaofahamu matumizi ya whatsapp, screen shot hii ilipaswa kutoka kwenye simu yangu, kwa maana nyingine ni mimi mwenyewe ndiye chanzo cha jambo hili.

2. Wanaonifahamu whatsapp sio moja ya njia yangu ya mawasiliano, situmii simu aina ya samsung ambayo ndiyo inayoonekana ilikuwa inatumika katika mawasiliano hayo,na pia siifahamu na wala sijawahi kuwa na namba ya Airtel ya Ridhiwani.

3. Ukiiangalia Lugha na aina ya uchaguzi wa maneno uliotumika si aina yangu ya uandishi na maneno hata ambayo huwa nayatumia katika mazungumzo ya kawaida,mtu yoyote anayejua siasa atatambua mazungumzo hayo hayana mantiki yanaongelea mambo mengi na watu wengi kwa wakati mmoja.

4.Tarehe 5 April nilikuwa kwenye hall of fame Chuo kikuu Mzumbe na si Chalinze nilikokuwa tarehe 2,3 na 7. Muda wa ujumbe unatofautiana sana 5 am, 6.30am na 2.32pm.

Screenshots zinaonyesha kwamba majadiliano hayo yalifanyika tarehe 5 April ambayo mimi nilikuwa tayari Chuo Kikuu Mzumbe.

Mimi niliondoka Dar kwenda Chalinze rasmi siku ya tarehe 2 nikitokea katika shughuli za ugawaji wa madawati katika shule ya Sekondari Pugu  ambapo nilikuwepo huko tangu asubuhi bila kupitia sehemu yoyote na niliongozana na MNEC Anthony Mavunde kwa kupitia njia ya kisarawe ili kukwepa foleni. Na tarehe 7 nilienda tena Chalinze kusherehekea ushindi.

5. Jambo hili ni rahisi sana kulitengeneza kwa simu mbili na kusave majina unayotaka na unawezo hata wa kutoa ya upande wa pili inayoonyesha jina langu.Matumizi haya ya teknolojia ni vyema yatumike katika mambo ya msingi badala ya kujaribu kuleta fitna zisizo na maana na kujaribu kuwapa watu tabia ambazo hawajawahi kuwa nazo.

6. Ushauri wangu ni kwa kila mmoja wetu hasa wanasiasa kuwa makini na kuepuka kufitinishwa kwa fitina nafuu kama hii. Kwa jambo lilozungumzwa kwanza wakati bado na pili wanasiasa wa ngazi yangu na Ridhwan si wakulijadili jambo kubwa namna hiyo kwa hoja dhaifu hivyo na tena  kwenye whatsapp.
 
JERRY SILAA.


PICHA 7 ZA HARUSI YA PRODYUZA P-FUNK ZIPO HAPA

0 comments

Screen Shot 2014-04-20 at 12.22.00 AM
‘Finally I made the big move’ ni moja ya caption za picha alizoweka Producer huyu ambae mikono na akili yake vimetumika sana kuuinua muziki wa bongofleva toka inaanza enzi hizo na kina Juma Nature na wengine.
Screen Shot 2014-04-20 at 12.22.30 AM
Screen Shot 2014-04-20 at 12.23.29 AM
Screen Shot 2014-04-20 at 12.23.45 AM Screen Shot 2014-04-20 at 12.23.56 AM Screen Shot 2014-04-20 at 12.24.12 AM Screen Shot 2014-04-20 at 12.24.21 AM
Picha hii na nyingine zimetoka kwa jestina-george.com zikiwa ni Exlcusive kwake
Picha hii na nyingine zimetoka kwa jestina-george.com zikiwa ni Exlcusive kwake
Mkurugenzi na uongozi wa Masama Blog pia tunakutakia kila la kheri katika maisha haya mapya,Mwenyezi Mungu awatangulie.